Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 12:56

Hamas inajiandaa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano na kuwaachilia mateka


Bango linaloonyesha picha za mateka wanaoshikiliwa na Hamas.
Bango linaloonyesha picha za mateka wanaoshikiliwa na Hamas.

Vyanzo ndani ya makundi ya wanamgambo wa Palestina huko Gaza Jumapili vimesema kwamba Hamas imewataka kukusanya taarifa kuhusu mateka wanaoshikiliwa na makundi hayo kwa ajili ya maandalizi ya makubaliano ya kusitisha mapigano na kuwaachilia mateka na Israel.

Hamas imeyaambia matawi yake ikiwemo Palestinian Islamic Jihad, the Popular Front and the Popular Resitance Committees kuandaa taarifa iwapo mateka bado wako hai au wamefariki, vyanzo hivyo vimeiambia AFP.

Wakati wa shambulizi la kushtukiza la Hamas la Oktoba 7, 2023 dhidi ya Israel, kundi hilo la wanamgambo na washirika wake waliwachukua mateka watu 251.

Jumla ya mateka 96 bado wako Gaza, ikiwemo 34 ambao Jeshi la Israel limethibitisha wamefariki.

Forum

XS
SM
MD
LG