Polisi nchini Korea Kusini wamesema wamepeleka maafisa kufanya upekuzi katika ofisi ya rais Yoon Suk Yeol leo Jumatano, kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea baada ya kutangaza matumizi ya sheria ya kijeshi.
Russia imesema kwamba uhusiano wake na Marekani ni mbaya kiasi kwamba raia wake wameshauriwa kutosafiri kwenda Marekani, Canada au baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya kwa sababu wanakabiliwa na hatari ya kuandamwa na mamlaka za Marekani.
Waziri wa Afghanistan anayehusika na wakimbizi aliuawa Jumatano katika mlipuko kwenye afisi za wizara hiyo katika mji mkuu Kabul, chanzo cha serikali kimeiambia AFP.
Usafirishaji haramu wa binadamu umeongezeka sana kutokana na mizozo, majanga yanayosababishwa na hali ya hewa na mizozo ya dunia, kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa Jumatano.
Sudan, kwa mwaka wa pili mfululizo imeorodheshwa miongoni mwa mataifa yanayokumbwa na mzozo mbaya wa kibinadamu duniani katika ripoti iliyotolewa Jumatano na shirika la hisani la International Rescue Committee (IRC), ikifuatiwa na Gaza na Ukingo wa Magharibi, Myanmar, Syria na Sudan Kusini.
Maombi yanaongezeka kutoka kote duniani kuyalinda makazi na dini za walio wachache nchini Syria, kufuatia kuondolewa kwa utawala wa Rais Bashar al-Assad, na waasi wa Kiisalamu.
Maafisa wa Somali wamesema Jumanne kwamba Rais wao Hassan Sheikh Mohamud na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, wamepanga kukutana ana kwa ana mjini Ankara, Uturuki.
Mahakama ya Katiba ya Zambia Jumanne kwa kauli moja imetoa maamuzi kuwa rais wa zamani Edgar Lungu hawezi kuwania kugombea kwenye uchaguzi wa 2026 kwa kuwa tayari amehudumu mihula miwili.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin Jumanne amethibitisha tena kile alichokiita uungwaji mkono usiotetereka wa ulinzi kwa Japan na Korea Kusini katika kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na China katika eneo la East China Sea.
Waziri mkuu wa israel Benjamin Netanyahu amefika katika mahakama ya Tel Aviv Jumanne kwa mara ya kwanza katika kesi ya rushwa inayomkabili kwa muda mrefu.
Familia za wafungwa wa Syria Jumatatu zilikuwa zinazunguka kwenye vyumba vichafu katika jela ya Sednaya mjini Damascus kujaribu kuona dalili za kuwpata jamaa zao waliofungwa kwa muda mrefu pale milango ilipofunguliwa na waasi.
Kiongozi wa waasi nchini Syria Abu Mohammed al-Golani kwa mara ya kwanza Jumatatu amekutana na waziri mkuu anayeondoka madarakani kufuatia kusonga mbele kwa haraka kwa waasi ambao walimuondoa rais Bashar al Assad.
Pandisha zaidi