Waziri wa Ulinzi, Lloyd Austin pia alikutana na Waziri Mkuu wa Japan Shigeru Ishiba Jumanne kujadiliana kuhusu maswala ya kieneo.
Austin alikuwa Japan siku ya Jumapili usiku, baada ya kuahirisha safari iliyopangwa ya Korea Kusini, kufuatia jaribio lililoshindwa wiki iliyopita la Rais Yoon Suk Yeol kuweka amri ya kijeshi.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani amesema “sasa tuko wazi kuhusu changamoto za amani na utulivu katika eneo hili na kote ulimwenguni”
“Hii ni pamoja na tabia za kulazimisha za watu wa Jamhuri ya China katika East China Sea na South China Sea na kwingineko katika eneo hilo” ameongeza.
Forum