“Tunadhibitisha kuwa kuna takriban wanajeshi 10,000 wa Korea Kaskazini ndani ya Russia, na taarifa za hivi karibuni zinaonyesha kuwa karibu 8,000 miongoni mwao wamepelekwa kwenye mkoa wa Kursk,” amesema waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken. Blinken na mwenzake wa Ulinzi Lloyd Austine waliongoza kikao na wenzao wa Korea Kusini Cho Tae-Yul na Kim Yong–hyun mtawalia hapa Washington DC Alhamisi.
Wakati wa kikao chao walizungumzia tishio la usalama wakati wakiangalia kwa karibu upelekaji wa maelfu ya wanajeshi wa Korea Kaskazini nchini Russia. Austin wakati akizungumza na wanahabari akiwa pamoja na mawaziri hao wenzake alisema kuwa,” Kwa maoni yetu ni kwamba vikosi vya Rais Vladimir Putin vimetoa mafunzo ya kutumia silaha za anga zisizo na rubani kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini.” Aliongeza kusema kuwa Putin pia ametoa sare za wanajeshi wa Russia pamoja na vifaa kwa wanajeshi hao wa Korea Kaskazini.
Forum