Netanyahu aliwasili majira ya asubuhi wakati waandamanaji wachache wakiwa wamekusanyika nje, baadhi yao ni wafuasi wake na wengine wanamtaka afanye mashuriano zaidi ya kuachiliwa kwa mateka 100 ambao bado wanashikiliwa na Hamas huko Gaza.
Israel imekuwa katika vita huko Gaza dhidi ya kundi la wanamgambo wa Palestina kwa zaidi ya mwaka mmoja, hali ambayo ilifanya Netanyahu kupewa uchelewesho wa muda kufika katika mahakamani.
Lakini alhamisi iliyopita, majaji waliamua kwamba ni lazima aanze kutoa ushahidi.
Ameshtakiwa kwa rushwa, ubadhirifu na kuvunja uaminifu, Netanyahu atatoa ushajidi mara tatu wiki hii, mahakama imesema, licha ya vita vya Gaza na uwezekano wa vitisho vipya vinavyotokana na machafuko makubwa mashariki ya kati ikiwa ni pamoja na nchi Jirani ya Syria.
Forum