Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 07:40

Watu kadhaa wauwawa na Iasrael, Lebanon


Dazeni ya watu wameripotiwa kuuwawa na mashambulizi ya Israel, mashariki mwa Lebanon, Alhamisi.

Gavana wa jimbo la Baalbek-Hermel, amesema kwamba watu 47 waliuwawa na wengine 22 kujeruhiwa katika eneo lake kwa mashambulizi hayo.

Mashambulizi ya Alhamisi, yamefanyika siku moja baada ya mwakilishi wa Marekani, Amos Hochstein, kuondoka Lebanon kwenda Israel, katikati ya msukumo wa kusimamishwa kwa mapigano ya vita vya Israel na kundi la wanamgambo wa Lebanon, Hezbollah.

Hockstein alikutana na waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, waziri wa ulinzi Israel Katz, lakini hakukuwa na ripoti za haraka kutoka kwenye mkutano huo.

Hata hivyo, afisa mwandamizi wa Lebanon, ameiambia Reuters kwamba nchi yake inatarajiwa mabadiliko katika mapendekezo kuhakikisha kuondoka kwa vikosi vya Israel nchini Lebanon.

Forum

XS
SM
MD
LG