Israel imesema Jumapili kuwa mwili wa kiongozi wa dini raia wa Israel mwenye asili ya Moldova ambaye alipotea akiwa Umoja wa Falme za Kiarabu umepatikana baada ya kuuawa katika kile Israel ilichokielezea kuwa ni tukio la kutisha la kinyama dhidi ya Wayahudi.
Taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu imesema Israel itachukua hatua kwa kila njia kutafuta haki na wahalifu waliohusika na kifo chake. Hakuna maoni ya haraka kutoka UAE.
Zvi Kogan, mwenye miaka 28, kiongozi wa Orthodox ambaye alipotea Alhamisi alikuwa na duka la vyakula vya Kosher mjini Dubai ambapo Waisraeli wamefurika kufanya biashara na utalii tangu nchi hizo mbili zilipoanzisha uhusiano wa kidiplomasia kupitia mkataba wa Abraham wa 2020.
Makubaliano hayo yalifanyika zaidi ya mwaka mmoja kukiwa na mivutano ya kikanda baadaye kulitokea shambulio la Hamas la Oktoba 7, mwaka 2023 huko kusini mwa Israel. Lakini mashambulizi ya Israel ya kulipiza kisasi huko Gaza na uvamizi wake kwa Lebanon baada ya miezi kadhaa ya mapigano na kundi la wanamgambo wa Hezbollah, yamechochea hasira miongoni mwa wa-Imirati, raia wa Kiarabu na watu wengine wanaoishi UAE.
Forum