Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 07:24

Israel yafikia sitisho la mapigano na kundi la Hezbollah la Lebanon


Shughuli za uokozi kwenye mji mkuu wa Lebanon, Beirut, kufuatia mashambulizi ya awali ya Israel. Picha ya maktaba
Shughuli za uokozi kwenye mji mkuu wa Lebanon, Beirut, kufuatia mashambulizi ya awali ya Israel. Picha ya maktaba

Israel Jumanne jioni imekubali kusitisha mapigano dhidi ya kundi la Hezbollah la Lebanon, hatua ambayo huenda ikamaliza vita vilivyodumu kwa mwaka mmoja, iwapo sitisho hilo litaanza kutekelezwa Jumatano.

Licha ya hilo, jeshi la Israel liliendelea kushambulia ngome za Hezbollah kusini mwa Lebanon, wakati waziri mkuu wa Benjamin Netanyahu akiambia televisheni ya kitaifa kuwa angeomba mawaziri wa Usalama kuidhinisha sitisho hilo la mapigano, ingawa hilo lilifanyika muda mfupi baadaye.

Marekani pamoja na Ufaransa wamekuwa kwenye mstari wa mbele kwenye mazungmzo kuelekea sitisho hilo. Kwenye Ikulu ya Marekani, Rais Joe Biden alitaja sitisho hilo la mapigano kuwa “hatua muhimu,” kuelelea kumalizwa kwa ghasia Mashariki ya Kati. Alisema kuwa Iran na washirika wake Hebollah na wanamgambo wa Hamas wamelipa gharama kubwa kwenye mapigano yaliodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja dhidi ya vikosi vya Israel.

Aliongeza kusema kuwa mkataba kati Israel na Hezbollah utakuwa wa kudumu. Hata hivyo Biden alionya kuwa, “Nataka kuweka bayana kwamba iwapo Hezbollah au mwingine yeyote atavunja mkataba huo na kuwa tishio kwa Israel, basi Israel ina kila haki ya kujilinda, kwa mujibu wa sheria za kimataifa ,sawa na taifa lolote linalotishiwa na kundi la kigaidi.”

Forum

XS
SM
MD
LG