Mgombea wa chama kikuu cha upinzani nchini Namibia, Panduleni Itula, Jumamosi alisema kwamba chama chake hakitatambua matokeo ya uchaguzi wa rais wenye utata uliogubikwa na vurugu na madai ya wizi wa kura.
Mkuu wa masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa Jumuia ya kimataifa kuchukua hatua za haraka ili kushughulikia mzozo wa Sudan unaozidi kuwa mbaya, akisisitiza mateso kwa mamilioni ya watu waliokoseshwa makazi kutokana na mzozo huo.
Rais wa Kenya Dr. William Ruto, amesema kwamba ni jukumu la pamoja la viongozi wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhakikisha kwamba kanda nzima ina usalama na utulivu.
Waasi nchini Syria wamedhibiti sehemu kubwa ya mji wa Aleppo ambao ndio mji mkubwa zaidi nchini Syria.
Hesabu ya kura inaendelea nchini Iceland katika uchaguzi wa bunge uliofanyika leo Jumamosi, baada ya kutokea hali ya kutoelewana kuhusu maswala ya uhamiaji, sera ya nshati na uchumi.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema kwamba hatua ya nchi hiyo kuruhusiwa kuwa mwanachama wa NATO inaweza kumaliza kile amekitaja kama hatua moto ya vita vya Russia.
Jeshi la Israel limesema kwamba limeua Mpalestina anayeshutumiwa kushiriki katika shambulizi la Oktoba 7 dhidi ya Israel.
Watu 107 wamekamatwa nchini Georgia leo Jumamosi katika siku ya pili ya maandamano ya kupinga uamuzi wa serikali kuchelewesha mazungumzo kuhusu mapendekezo ya nchi hiyo kujiunga na Umoja wa Ulaya.
Takriban watu 18 walifariki dunia wakati boti iliyokuwa imebeba abiria ilikuwa inaelekea sokoni katika mkoa wa Far North nchini Cameroon ilipopinduka, afisa utawala wa eneo hilo alisema Ijumaa
Idadi ya waliofariki dunia kutokana na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa mashariki mwa Uganda imepanda hadi 17
Bunge la Uingereza limepiga kura kuukubali mswada wa kuhalalisha usaidizi wa kifo siku ya Ijumaa, na kufungua nafasi kwa mjadala zaidi wa miezi kadhaa kuhusiana na suala ambalo limeigawa nchi na kuzua maswali kuhusiana na kiwango cha uuguzi na uponyaji.
Waasi wa Syria wamevamia mji wa pili kwa ukubwa nchini Syria wa Aleppo, baada ya kulipua mabomu mawili ya kwenye gari wakipamba ba majeshi ya serikali siku ya Ijumaa, kulingana na mfuatiliaji wa vita vya Syria na wapiganaji.
Pandisha zaidi