Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 13, 2025 Local time: 20:09

Zelenskyy anaamini vita vitamalizika Ukraine ikijiunga na NATO


Rais wa Ukriane Volodymyr Zelenskyy katika kikao na waandishi wa habari mjini Kyiv, Okt 21 2024
Rais wa Ukriane Volodymyr Zelenskyy katika kikao na waandishi wa habari mjini Kyiv, Okt 21 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema kwamba hatua ya nchi hiyo kuruhusiwa kuwa mwanachama wa NATO inaweza kumaliza kile amekitaja kama hatua moto ya vita vya Russia.

Katika mahojiano na shirika la habari la Sky News, Zelenskyy amependekeza kwamba anaweza kukubali kusitisha vita iwapo sehemu za Ukraine ambazo hazijachukuliwa, zitadhibitiwa na NATO, na iwapo hatua ya kujumulishwa katika muungano wa ulinzi wa NATO, itatambua mipaka ya kimataifa ya Ukraine.

Russia iliikamata sehemu ya Ukraine ya Crimea mwaka 2014 na imekuwa ikikalia asilimia 20 ya Ukraine tangu ilipoivamia nchi hiyo Februari 2022.

Hayo yanajiri wakati rais mteule wa Marekani Donald Trump amekosoa msaada wa mabilioni ya dola unaotolewa kwa Ukraine tangu Russia ilipoivamia nchi hiyo.

Trump vile vile amesema kwamba atamaliza vita hivyo katika muda wa saa 24 atakapoingia White House, hatua ambayo imetafsiriwa kumaanisha kwamba Ukraine italazimika kuachilia sehemu ambazo Russia inazikalia.

Mapema wiki hii, Trump amemteua Keith Kellogg, luteni jenerali mstaafu, ambaye amekuwa mshauri wa Trump wa mambo ya ulinzi, kuwa mjumbe wake maalum kwa ajili ya Ukraine na Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG