Hali hiyo ya kutoelewana ilipelekea Waziri Mkuu Bjarni Benediktsson kuvunja serikali ya muungano na kuitisha uchaguzi wa mapema.
Hii ni mara ya sita Iceland inaadaa uchaguzi mkuu tangu mgogoro wa uchumi wa mwaka 2008 ulioharibu uchumi wa kisiwa hicho cha Atlantiki kaskazini na kupelekea mgogoro wa kisiasa.
Ukusanyaji maoni unaonyesha kwamba huenda nchi hiyo ikaingia katika mgogoro mkubwa wa kisiasa, kutokana na vyama vyote vitatu vinavyotawala kukosa uungwaji mkono wa wapiga kura.
Benediktsson, ambaye aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu mwezi Aprili baada ya mtangulizi wake kujiuzulu, amekuwa na wakati mgumu kusimamia serikali iliyo thabiti ya chama chake cha Conservative Progressive Party na Green Movement.
Iceland, yenye idadi ya watu 400,000 inajivunia kwa mfumo thabiti wa demokrasia, ikijitambua kama nchi yenye mfumo madhubuti wa utawala wa bunge.
Forum