Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:17

Idadi ya waliofariki  kutokana na maporomoko ya ardhi Uganda yaongezeka

Waziri Mkuu wa Uganda Robinah Nabbanja akitembelea eneo la maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyozika nyumba nyingi katika vijiji kadhaa wilayani Bulambuli, Uganda Novemba 29, 2024. REUTERS

Idadi ya waliofariki dunia  kutokana na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa mashariki mwa Uganda imepanda hadi 17

Idadi ya waliofariki dunia kutokana na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa mashariki mwa Uganda imepanda hadi 17, msemaji wa serikali alisema Ijumaa, huku wengine zaidi ya 100 wamepotea.

Maporomoko hayo ya ardhi yalitokea siku ya Jumatano katika wilaya ya Bulambuli, kiasi cha kilomita 300 mashariki mwa mji mkuu Kampala, na darzeni ya nyumba kufukiwa katika vijiji kadhaa.

Picha za kwenye televisheni nchini humo zilionyesha maeneo makubwa yakiwa yamefunikwa na matope mazito ambako nyumba na shule zilikuwepo. Walionusurika walikuwa wakilia kwa kupoteza wapendwa wao huku waokoaji wakichimba kwenye tope kuwatafuta manusura.

Forum

XS
SM
MD
LG