Rais Joe Biden wa Marekani ameanza ziara ya siku mbili nchini Angola kwa mazungumzo na mwenyeji wake Rais Joao Lourenco, juu ya ushirikiano wa kibiashara na uchumi.
Zaidi ya watu 100 wanahofiwa kupotea na wengine 17 wamefariki baada ya maporomoko ya ardhi ya Jumatano kwenye Mlima Elgon
"Tutafanya Chuma cha Marekani kuwa na nguvu na bora kwa mara nyingine, na hili litafanyika haraka, nitazuia mpango huu kutokea".
Vitisho vya Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, vya kuweka ushuru vimeleta mvutano baina ya Mexico na Canada, baada ya maafisa wa Canada kusema matatizo ya mpaka wa mataifa hayo mawili hayapaswi kulinganishwa.
Mkuu wa shirika la watoto la Umoja wa Mataifa, Jumatatu amesema kwamba watoto wanajumuisha takriban nusu ya wanachama wa makundi yenye silaha ya Haiti, na kutoa mwito wa kulindwa kwao.
Utawala wa Rais Biden, wa Marekani, Jumatatu umetangaza kuweka vikwazo kadhaa vipya kwa bidhaa kwenda China, vikizuia kuuzwa kwa vifaa muhimu vya teknolojia za viwandani, na vile vikubwa vya kuweka kumbukumbu za kompyuta.
Serekali ya visiwa vya Ugiriki vya Rhodes, na Lemnos, imetangaza hali ya dharura Jumatatu, baada ya dhoruba kukumba visiwa hivyo na kusababisha vifo vya watu wawili na kufanya uharibifu mkubwa.
Wizara ya afya ya Lebanon ilisema shambulizi la Israel Jumatatu lilimuuwa mtu mmoja kusini mwa Lebanon, huku jeshi la Lebanon likisema shambulio la Israel lilimjeruhi mwanajeshi katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.
Rais wa Chad Mahamat Deby alisema uamuzi wa kusitisha mkataba wa kijeshi wa nchi hiyo na Ufaransa umechukuliwa kwa sababu umepitwa na wakati katika matamshi yake ya kwanza hadharani tangu kutangazwa kwa mshangao wiki iliyopita.
Uamuzi wa kutatanisha wa refa katika mechi ya mpira wa miguu ulizua vurugu na mkanyagano katika mechi moja ya soka kusini mashariki mwa Guinea, na kuuwa watu 56 kulingana na idadi ya awali, serikali ilisema Jumatatu.
Ziara ya Rais Joe Biden nchini Angola – ni ya kwanza kufanywa na Rais wa Marekani katika taifa hilo la kusini magharibi mwa Afrika – ziara hiyo inahusu zaidi ujenzi wa njia ya reli ambayo itasafirisha madini yenye thamani kutoka Katikati mwa bara hilo kupitia bandari ya Angola.
Rais wa Marekani, Joe Biden, Jumapili, alifanya kumbukumbu ya UKIMWI, katika bustani ya kusini mwa White House kwa mara ya kwanza, ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani.
Pandisha zaidi