Wizara ya afya ya Lebanon ilisema shambulizi la Israel Jumatatu lilimuua mtu mmoja kusini mwa Lebanon, huku jeshi la Lebanon likisema shambulio la Israel lilimjeruhi mwanajeshi katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.
Jeshi la Israel halikutoa maoni yake mara moja kuhusu mashambulizi hayo.
Mashambulizi hayo yanakuja siku chache baada ya Israel na Hezbollah kukubaliana kusitisha mapigano, na hivyo kusimamisha mapigano ya miezi 14 yaliyozuka kufuatia shambulio la mshirika wa Hezbollah Hamas dhidi ya Israel.
Wakati wa shambulio hilo, Hamas iliua takriban watu 1,200 na kuwachukua mateka wengine 250. Bado kuna mateka wapatao 100 wanaozuiliwa katika Ukanda wa Gaza, huku takriban theluthi moja wakiaminika kuwa wamekufa.
Forum