Jumatatu, rais wa Mexico alipinga matamshi hayo ambayo yalitolewa baada ya mkutano baina ya Trump, na waziri mkuu wa Canada, Justin Trudeau. Rais Claudia Sheinbaum, wa Mexico amesema taifa lake lazima liheshimiwe na washirika wake wa kibiashara.
Hii ni baada ya balozi wa Canada, Marekani Kristen Hillman, Jumapili kuiambia The Associated Press kwamba mipaka yake na Marekani ni tofauti sana ikilinganishwa na ile ya Mexico na kwamba ni jambo linaloeleweka.
Rais mteule wa Marekani Trump, ametishia kuongeza ushuru kwa asilimia 25 kwa bidhaa kutoka Canada na Mexico mpaka pale zitakapo shughulikia masuala ya wahamiaji na dawa za kulevya.
Forum