Mwaka 2024 ulishuhudia kuongezeka kwa shughuli za kisiasa barani Afrika, vyama vilivyotawala kwa muda mrefu vikipitia mtihani mkubwa kushinda uchaguzi.
Mshauri wa Benki ya Dunia Brian Pinto na mkuu wake wa masuala ya Uchumi, Indermit Gill wanatathmini ya DSA
Baraza la kikatiba nchini Msumbiji imeidhinisha ushindi wa chama kinachotawala cha Frelimo, baada ya uchaguzi wa mwezi Oktoba ambao umesababisha maandamano makubwa kutoka kwa makundi ya upinzani yanayodai kwamba kulikuwa na wizi wa kura.
Serikali ya China Jumapili imelalamikia tangazo la karibuni la Marekani la kutoa misaada ya kijeshi pamoja na kuiuzia Taiwan silaha, ikionya Marekani kwamba inacheza na moto.
Waziri mkuu wa Albania Edi Rama, amesema Jumapili kwamba hatua ya kupigwa marufuku kwa jukwaa la TikTok na serikali yake siku moja kabla “haikuwa ya kushtukiza na wala siyo kutokana na tukio moja.”
Huenda takriban watoto 3,104 kutoka makabila ya jadi walikufa kwenye shule za bweni Marekani baada ya kuondolewa kutoka kwenye familia zao kwa nguvu wakilazimishwa kuingia kwenye mfumo wa kawaida wa maisha, gazeti la The Washington Post limeripoti Jumapili.
Mamlaka za Ujerumani zilipokea taarifa za tahadhari mwaka jana kuhusu mshukiwa wa shambulizi la gari kwenye soko la Christmas, ofisi ya serikali imesema Jumapili, huku maelezo zaidi yakitolewa kuhusu watu watano waliouawa katika shambulizi hilo.
Kiongozi mpya wa Syria Ahmed al-Sharaa Jumapili amewambia viongozi wa jamii ya walio wachache nchini Lebanon ya Druze kwamba nchi yake haitoingilia kati kwa nia mbaya katika masuala ya Lebanon na kwamba itaheshimu uhuru wa jirani yake.
Polisi nchini Nigeria Jumapili wamesema idadi ya vifo katika matukio mawili ya mkanyagano nje ya vituo vya kugawa chakula kwa watu maskini imeongezeka hadi 32.
Mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza usiku kucha hadi Jumapili yameua watu 20 wakiwemo watoto watano, maafisa wa idara za matibabu za Palestina wamesema.
Baraza la Seneti la Marekani mapema Jumamosi asubuhi limepitisha mswada wa bajeti kuifadhili serikali kuu ya Marekani hadi mwezi Machi mwakani.
Wajerumani Jumamosi wameomboleza waathirika wa shambulizi lililofanywa na daktari raia wa Saudi Arabia ambaye aliendesha kwa makusudi gari lake ndani ya umati wa watu na kuwagonga wale waliokuwa kwenye soko la kuuza bidhaa za siku kuu ya Christmas, na kuua watu watano.
Pandisha zaidi