Venâncio Mondlane, ambaye alimaliza katika nafasi ya pili kulingana na hesabu rasmi ya tume ya uchaguzi, amekuwa akitaka wafuasi wake kujitokeza mitaani na barabarani kwa maandamano, akida uchaguzi ulijaa udanganyifu.
Uchaguzi ulifanyika Oktoba 9 katika nchi hiyo yenye jumla ya watu milioni 35.
Mondlane, anaishi uhamishono baada ya kutoroka msumbizi. Alidai kwamba maafisa wa polisi walikuwa wanatishia Maisha yake. Walinzi wake wawili walipigwa risasi na kuuawa mwezi Oktoba.
Ameandika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii akionywa uwezekano mkubwa wa kutokwa maandamano iwapi matokeo ya uchaguzi hayatabatilishwa.
Wakaazi wa Maputo wamesalia nyumbani, Barabara, miji imesalia tupu licha ya maandalishi ya sherehe za krisimasi. Baadhi ya waandamanaji wameonekana leo mjini Maputo wakiziba Barabara kuzuia magari.
Maandamano yalianza Oktoba 21. Mondlane ameambia vyombo vya habari kwamba hawezi kabisa kukubali matokeo ya uchaguzi ambapo mgombea wa chama kilicho madarakani cha Frelimo, Daniel Chapo, alipata asilimia 71 ya kura. Mondlane alipata asilimia 20.
Utata wa matokeo ya uchaguzi
Chama cha Frelimo kimetawala Msumbiji kwa miaka 49, tangu mwaka 1975 ilipopata uhuru kutoka kwa Ureno
Tume ya uchaguzi imepuuzilia mbali madai ya Mondlane kwamba kulikuwa na wizi wa kura. Waangalizi wa kimataifa wanakubaliana na madai ya Mondlane kwamba uchaguzi ulijaa udanganyifu wakati wa hesabu ya kura. Mondlane anadai kwamba alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 53.
Chama cha Podemo, chenye ushirikiano na Mondlane, kinasisitiza kwamba kilipata viti vya bunge 138 na wala sio 31 ilivyotangwa na tume ya uchaguzi.
Bunge la Msumbiji lina viti 250.
Maandamano ya zaidi ya miwezi miwili yamepelekea polisi kukabiliana na waandamanaji kwa wiki kadhaa. Watu 130 wamethibitishwa kuuawa.
Inadaiwa kwamba waliouawa walipigwa risasi na polisi lakini kamanda wa polisi Bernadino Rafael ameambia waandishi wa habari kwamba polisi wamekuwa wakijilinda dhidi ya waandamanaji wanaowashambulia.
Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis ametoa ujumbe wa kutaka viongozi wa Msumbiji kufanya mazungumzo kwa ajili ya utulivu na watu wa Msumbiji.
Wito wa kutaka mazungumzo
Kuna ripoti kwamba Mondlane amekuwa akifanya mazungumzo na rais Filipe Nyusi lakini hakuna taarifa za kutosha kuhusu mambo wanayozungumzia.
Nyusi alihutubia taifa alhamisi usiku na kuahizi kwamba ataondoka madarakani mwezi Januari anavyohitajika kikatiba.
Baadhi ya waangalizi kama wa jumuiya ya nchi za madola wameambia vyombo vy ahabari kwamba iliwashitua sana kwamba Frelimo kilipata asilimia 70 ya kura, lakini pia ni vigumu kujua kama kweli Venancio Mondlane alishinda uchaguzi huo.
Majaji wanne kati ya saba, katika baraza la kikatiba, walichaguliwa na wabunge wa chama kinachotawala cha Frelimo. Mwenyekiti wa baraza hilo aliteuliwa na rais Filipe Nyusi.
Forum