Jumamosi Rais wa Marekani Joe Biden alitangaza utoaji wa hadi dola milioni 571 kupitia wizara ya Ulinzi, kwa ajili ya vifaa na huduma za kijeshi pamoja na mafunzo ya kijeshi kwenye kisiwa cha Taiwan kinachojitawala, na ambacho Beijing inadai ni himaya yake.
Kwenye taarifa tofauti, wizara ya Ulinzi ya Marekani ilisema mwishoni mwa wiki kwamba uuzaji wa silaha za kijeshi wa dola milioni 295 kwa Taiwan tayari umeidhinishwa. Taarifa kutoka wizara ya mambo ya nje ya China imeisihi Marekani isitishe kutoa silaha kwa Taiwan pamoja na kusitisha kile imekitaja kuwa “ hatua hatari zinazohujumu amani na uthabiti kwenye Mlango wa bahari wa Taiwan.
Msaada wa kijeshi pamoja na silaha kutoka Marekani zinalenga kuisaidia Taiwan kujilinda dhidi ya mashambulizi ya China. Tangazo la msaada wa kijeshi wa dola milioni 571 kwa Taiwan umefuatia hatua ya Biden ya kuidhinisha msaada mwingine wa dola milioni 567 mwishoni mwa Septemba. Msaada huo utatumika kununua takriban mifumo 300 ya mawasiliano ya kijeshi miongoni mwa vifaa vingine.
Forum