Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:27

Marekani imeidhinisha uuzaji wa silaha kwa Taiwan


Rais wa taiwan Lai Ching-te wakati wa ziara katika kambi ya kijeshi baada ya China kufanya mazoezi ya kijeshi Taoyuan
Rais wa taiwan Lai Ching-te wakati wa ziara katika kambi ya kijeshi baada ya China kufanya mazoezi ya kijeshi Taoyuan

Pentagon imesema kwamba Marekani imeidhinisha uuzaji wa silaha zenye thamani ya dola bilioni 2 kwa Taiwan, ikiwemo mfumo wa ulinzni wa anga.

Hii ni mara ya kwanza Marekani imetoa mfumo wa ulinzi wa anga kwa Taiwan. Mfumo huo ulifanyiwa majaribio nchini Ukraine.

Marekani inatakiwa kwa mujibu wa sheria, kuipatia silaha Taiwan kwa ajili ya kujilinda licha ya kutokuwepo uhusiano rasmi wa kidiplomasia, hatua ambayo kila mara imeikasirisha Beijing.

China inadai kisiwa cha Taiwan ni himaya yake, na imekuwa ikiimasrisha shughuli za kijeshi dhidi ya kisiwa hicho, ikiwemo kufanya mazoezi wiki iliyopita karibu na Taiwan.

Mazoezi hayo ya kijeshi yamekuwa ya pili tangu Lai Ching-te alipoingia madarakani kama rais wa Taiwan mwezi Mei.

Forum

XS
SM
MD
LG