Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:04

China yaishutumu Marekani kwa matumizi mabaya ya kanuni za biashara


Utengenezaji wa bidhaa za kielektroniki aina ya chips.
Utengenezaji wa bidhaa za kielektroniki aina ya chips.

Wizara ya Biashara ya China imeishutumu Marekani kwa kile imekitaja kama matumizi mabaya ya kanuni za biashara nje ya nchi.

Kauli hii imetolewa baada ya kampuni ya kutengeneza vifaa vya umeme ya Taiwan TSMC, kusitisha usafirishaji wa chips kwa China kutokana na shinkizo la Marekani.

Vyombo vya habari vinaripoti kwamba kampuni ya TSMC, ambayo ni kubwa duniani kwa utengenezaji wa Chips, ilisitisha usafirishaji wa vifaa hivyo kuanzia Jumatatu kutokana na ushawishi wa Marekani.

FILE - Nembo ya kampuni ya TSMC ikiwa katika maonyesho ya teknolojia huko Taiwan katika kituo cha kimataifa cha biashara, Oct. 14, 2022.
FILE - Nembo ya kampuni ya TSMC ikiwa katika maonyesho ya teknolojia huko Taiwan katika kituo cha kimataifa cha biashara, Oct. 14, 2022.

Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China He Yongqian, ameonya kwamba hatua ya kuvuruga biashara huru na kanuni za kibiashara zitaathiri maslahi ya wahusika wote na maendeleo ya teknolojia na ushirikiano wa kibiashara kote duniani.

Hatua hiyo ni ya hivi punde katika mgogoro wa teknolojia kati ya Marekani na China, ambapo Marekani inatafuta kulemaza uwezo wa China katika teknolojia ya akili mnemba – AI.

Forum

XS
SM
MD
LG