Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:01

Mkuu wa NATO asema ushirikiano wa Russia na Korea Kaskazini ni hatari


Mkuu wa NATO, Mark Rutte,  Alhamisi amesema ushirikiano wa kijeshi wa Korea Kaskazini na Russia, dhidi ya Ukraine, ni tishio linaloenea zaidi Ulaya na lazima lishughulikiwe kwa pamoja.

“Jukumu hili la Korea Kaskazini kimsingi linaonyesha jinsi nchi hizi zinavyofanya kazi pamoja na China, Korea Kaskazini, Russia na bila shaka, Iran,” Rutte aliwaambia waandishi wa habari kabla ya kukutana na viongozi wa Ulaya mjini Budapest.

Amesema hili ni tishio zaidi na sio tu kwa sehemu ya Ulaya ya NATO, lakini pia kwa Marekani, kwa sababu Russia inapeleka teknolojia ya kisasa kwa Korea Kaskazini ikiwa kama malipo ya msaada wa Korea Kaskazini katika vita dhidi ya Ukraine.

Rutte amesema ikiwa Russia, itafanikiwa Ukraine, itakuwa na ujasiri na vifaa bora zaidi, na hivyo kutoa tishio kubwa katika mipaka ya NATO na Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG