Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 10:47

Maafisa wa Marekani wanaeleza mtazamo wao kuhusu mkutano wa BRICS


Mkutano wa kundi la BRICS nchini Russia
Mkutano wa kundi la BRICS nchini Russia

Wachambuzi wanasema wanachama wa BRICS wanashughulikia masuala yanayoweza kuwaondolea ushawishi kutoka Magharibi.

Wakati maafisa wa Marekani wakielezea mtazamo kwamba mkutano wa kundi la BRICS katika mji wa Kazan nchini Russia haujitokezi kuwa hasimu wa kijiografia, wachambuzi wanasema wanachama wa BRICS wanashughulikia masuala ambayo yanaweza kuwaondolea ushawishi kutoka nchi za Magharibi.

Miongoni mwa mada zilizojadiliwa kati ya nchi wanachama Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini ni njia za kuanzisha mfumo mbadala wa malipo ambao hautategemea dola ya Marekani, sarafu ya kidijitali ya BRICS na njia mbadala ya taasisi za kifedha za Magharibi kama vile Shirika la Kimataifa la Fedha.

China, Russia na Iran, ni nchi ambazo zinakabiliwa na vikwazo vikali vya kibiashara vilivyowekwa na Marekani, zimekuwa na nia ya kuendeleza malengo ya BRICS na kuzuia kile wanachokiona kama vikwazo visivyo halali.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amesema katika mkutano wa BRICS kwamba ana maslahi yaliyo sawa. Tunakaribisha juhudi za kuongeza ushirikiano wa kifedha kati ya nchi za BRICS. Biashara katika sarafu za ndani na malipo rahisi ya mipakani yataimarisha ushirikiano wetu wa kiuchumi, alisema Modi.

Forum

XS
SM
MD
LG