Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:53

Taiwan yaona meli, na ndege za kijeshi za China katika himaya yake


Wizara ya ulinzi ya Taiwan, Jumapili imesema kwamba imeziona meli 35 za kijeshi za China, ikijumuisha za kijeshi na zakufyatua mabomu, zikiruka kusini mwa kisiwa hicho zikiwa njiani kufanya mazoezi katika bahari ya Pacific, kwa siku ya pili mfululizo ikiripoti matukio hayo.

China inaiona Taiwan inayo jiendesha kidemokrasia kama sehemu yake licha ya upinzani mkali wa serekali ya Taipei, kwa kawaida imekuwa ikituma jeshi lake angani na baharini karibu na kisiwa hicho ikitaka kuthibitisha madai ya umiliki wake.

Wizara ya ulinzi ya China haikujibu maombi ya kujibu kuhusiana na madai ya mazoezi yake yaliyo ripotiwa baada ya siku kadhaa kabla ya uchaguzi wa Jumanne wa rais wa Marekani.

Taiwan kisheria inaruhusiwa kujilinda yenyewe kwa ushirika na Marekani, na manunuzi ya silaha ikijumuisha mifumo ya dola bilioni mbili iliyo tangazwa mwezi uliopita na kuichukiwa Beijing.

Forum

XS
SM
MD
LG