Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Dunia wanakosoa tathmini ya kifedha ya Ethiopia iliyofanywa na Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) wakihoji iwapo uchambuzi ambao unasisitiza marekebisho ya deni la nchi unaweza kuwa una makosa.
Katika nakala ya ndani iliyoonekana na shirika la Habari la Reuters, mshauri wa Benki ya Dunia Brian Pinto, na mkuu wake wa masuala ya Uchumi, Indermit Gill wanatathmini Uchambuzi Endelevu wa Deni (DSA) katika tarehe za Julai iliyoandaliwa na IMF na wafanyakazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa(IDA), Benki ya Dunia kwa mataifa maskini sana.
Waandishi wanapendekeza kwamba kulingana na DSA, Ethiopia inakabiliwa na upungufu wa muda mfupi wa kifedha, na siyo tatizo la muda mrefu ambao linahitaji utatuzi, baina ya Serikali na wamiliki wa dhamana yake ya kimataifa yad ola bilioni moja.
Forum