Gavana wa Odesa, Oleh Kiper alisema kupitia mtandao wa Telegram vifusi vya Drone viliharibu majengo matano ya makazi.
Haya yanajiri mwaka mmoja baada ya serikali ya Sudan kusitisha uhusiano na jumuiya hiyo ya kikanda na kusitisha uanachama wake
Polisi nchini Kenya Jumatatu wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakiandamana kulalamikia visa vya utekaji nyara vya wale wanaoonekana kuipinga serikali.
Serekali ya Korea Kusini imesema takriban watu 179 wamefariki dunia baada ya ndege ya abiria kuungua Jumapili iliposerereka kwenye njia ya kurukia na kutua ndege na kugonga uzio wa zege.
Rais wa zamani Jimmy Carter, mkulima wa karanga na gavana wa jimbo la Georgia kabla ya kuwa rais, amefariki akiwa na umri wa miaka 100.
Rais wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter, mkulima wa karanga na gavana wa jimbo la Georgia kabla ya kuwa rais, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100.
Mateka walioshikiliwa huko Gaza waliteswa, ikiwemo unyanyasaji wa kingono na kisaikolojia, njaa, kuchomwa na kutopewa matibabu, kulingana na ripoti mpya ya wizara ya afya ya Israel, ambayo itawasilishwa huko Umoja wa Mataifa wiki hii ijayo.
Chad imefanya uchaguzi mkuu Jumapili unaoelezewa na serikali kama hatua muhimu kuelekea kumaliza utawala wa kijeshi, lakini uchaguzi huo umesusiwa na vyama vya upinzani.
Rais wa Azerbaijan Illham Aliyev Jumapili alisema kwamba ndege ya abiria ya nchi yake ambayo ilianguka wiki iliyopita na kuua watu 38, iliharibiwa na shambulizi la risasi kutoka Russia.
Maafisa wa Korea Kusini wamesema takriban watu 179 wamefariki wakati ndege ya abiria ilipoungua Jumapili baada ya kuserereka wakati wa kutua na kugonga uzio wa simenti.
Maelfu ya watu waliandamana Jumamosi katika mji mkuu wa Uturuki Ankara kuomba nyongeza ya kima cha chini cha mshahara, huku wakiimba nyimbo za kuitaka serikali kujiuzulu wakipeperusha bendera za upinzani na taifa.
Rais wa Russia Vladimir Putin Jumamosi amemuomba radhi rais wa Azerbaijan “kwa ajali hiyo mbaya” iliyotokea katika anga ya Russia ambapo ndege ya shirika la ndege la Azerbaijan ilianguka baada ya mifumo ya ulinzi wa anga kutumiwa dhidi ya ndege zisizo na rubani za Ukraine.
Pandisha zaidi