Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 04, 2025 Local time: 05:17

Jimmy Carter Afariki Dunia


Rais wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter, aliyefariki dunia Jumapili, Desemba 29, 2024. Alikuwa na umri wa miaka 100.
Rais wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter, aliyefariki dunia Jumapili, Desemba 29, 2024. Alikuwa na umri wa miaka 100.

Rais wa zamani Jimmy Carter, mkulima wa karanga na gavana wa jimbo la Georgia kabla ya kuwa  rais, amefariki akiwa na umri wa miaka 100.

Picha katika White House wakati wa maadhimisho ya miaka 100 toka kuzaliwa kwa Hayati Jimmy Carter, Rais wa zamani wa Marekani.
Picha katika White House wakati wa maadhimisho ya miaka 100 toka kuzaliwa kwa Hayati Jimmy Carter, Rais wa zamani wa Marekani.

Wakati Carter alipoapishwa kuchukua madaraka kama rais wa Marekani Januari 20, 1977, aliahidi “serikali nzuri kama walivyo watu wake. “

Alikabiliana na kipindi cha miaka minne iliyokuwa na misukosuko. Kupanda kwa mfumuko wa bei na ongezeko la ukosefu wa ajira ambao uligubikwa na vipaumbele vya ndani katika utawala wake.

Alisifika kwa sera za mambo ya nje kwa mkataba wa amani kati ya Misri na Israel na mkataba wa Mfereji wa Panama.

Hata hivyo, mzozo wa mateka nchini Iran ulitawala miaka yake ya mwisho katika White House na kuchangia kushindwa kwake katika uchaguzi mkuu wa 1980.

Waombolezaji wakiweka mashada ya maua katika kituo cha Rais Jimmy Carter, baada ya kutangazwa kifo cha chake, Jumapili, Desemba, 29, 2024.
Waombolezaji wakiweka mashada ya maua katika kituo cha Rais Jimmy Carter, baada ya kutangazwa kifo cha chake, Jumapili, Desemba, 29, 2024.

Lakini Carter alipenda kusema mwisho wa urais wake mwaka 1981 ulikuwa mwanzo wa maisha yake mapya, akisafiri duniani “kupambana na maradhi, kujenga matumaini, na kupigania amani.”

“Imetufungulia njia mimi na mke wangu, Rosalynn, enzi mpya ya msisimko na kutotabirika kwa matukio na changamoto na kuridhika,” aliiambia VOA.

Kama mkuu wa Carter Center, kina Carter walisafiri zaidi ya nchi 80 kufuatilia chaguzi zilizokuwa na matatizo, kupatanisha mizozo, na kupambana na magonjwa, harakati zake baada ya maisha ya White House hatimaye zilipelekea kushinda tuzo ya amani ya nobeli mwaka 2002.

“Naiangalia kazi ninayoifanya kwenye Carter Center kama muendelezo wa kile ambacho nilijaribu kama rais. Unajua, tumeleta amani kati ya Israel na Misri. Tulifungua uhusiano mkubwa sana na Latin Amerika kwa mkataba wa Mfereji wa Panama,” alisema.

“Kwahiyo kile ambacho nimekifanya tangu wakati huo imekuwa ni muendelezo.

Lakini sidhani kuna shaka yoyote wakati niliposhinda tuzo ya amani ya nobeli, kwa mfano, ilikuwa kwasababu ya kazi iliyofanywa na Carter Center.

Kwahiyo, ningependa kuwa na urithi ambao unazingatia amani na haki za binadamu, nina manaa, nani hataki hivyo?”

Safari ya Carter kwenda White House ilianzia katika mji mdogo wa Plains, Georgia, ambako alizaliwa Oktoba 1, 1924.

Baada ya kuhudumu kama afisa wa Jeshi la Navy la Marekani, ambako alisaidia kuendelea kusimamia manowari ya nyuklia ya Marekani baada ya vita vya pili vya dunia, Carter alirejea mji wa nyumbani kwake mwaka 1953 kusimamia biashara ya familia ya kilimo cha karanga.

Aliingia katika siasa katika miaka ya 1960, na kuhudumu kwa vipindi viwili kama mbunge wa Georgia kabla ya kuwa gavana wa 76 wa jimbo hilo kutoka mwaka 1971 mpaka 1975.

Forum

XS
SM
MD
LG