Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 04, 2025 Local time: 05:18

Mjumbe wa IGAD nchini Sudan anapanga ziara ya kuitembelea nchi hiyo


Picha kutoka Maktaba ikionyesha watu wa Sudan wanavyotaabika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Picha kutoka Maktaba ikionyesha watu wa Sudan wanavyotaabika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Haya yanajiri mwaka mmoja baada ya serikali ya Sudan kusitisha uhusiano na jumuiya hiyo ya kikanda na kusitisha uanachama wake

Mjumbe wa IGAD wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ajili ya Sudan amesema Jumatatu kuwa anapanga ziara mwezi ujao katika nchi hiyo iliyokumbwa na vita ambapo anajaribu kuwa mpatanishi.

Haya yanajiri mwaka mmoja baada ya serikali ya Sudan kusitisha uhusiano na jumuiya hiyo ya kikanda na kusitisha uanachama wake katika umoja huo.

Sudan imekuwa katika mgogoro uliosababisha vifo tangu mwezi Aprili mwaka jana ambapo kikosi cha wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) kinachoongozwa na Mohamed Hamdan Daglo maarufu kama Hemeti vinapigana na jeshi la Sudan linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan.

IGAD sambamba na Marekani na Saudi Arabia, mara kwa mara walijaribu kuwapatanisha kati ya majenerali hao wawili wanaohasimiana, lakini bila mafanikio.

Mwezi Januari jumuiya hiyo ilimwalika Daglo katika mkutano wa viongozi nchini Uganda, na kusababisha majibu ya hasira kutoka kwa wizara ya mambo ya nje katika serikali inayoungwa mkono na jeshi. Iliishutumu IGAD kwa kukiuka uhuru wa Sudan na kuweka mfano ulio hatari, ikisema itasitisha uanachama wake wa umoja huo.

Forum

XS
SM
MD
LG