Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 13:36

Rais wa Azerbaijan asema ndege ya nchi yake ilitunguliwa na shambulizi la Russia


Rais wa Azerbaijan Illham Aliyev
Rais wa Azerbaijan Illham Aliyev

Rais wa Azerbaijan Illham Aliyev Jumapili alisema kwamba ndege ya abiria ya nchi yake ambayo ilianguka wiki iliyopita na kuua watu 38, iliharibiwa na shambulizi la risasi kutoka Russia.

Amesema baadhi ya watu nchini Russia walisema uongo kuhusu sababu ya ajali hiyo.

Rais wa Russia Vladimir Putin Jumamosi alimuomba radhi Aliyev “kufuatia ajali hiyo mbaya” ya siku ya Jumatano katika anga ya Russia, wakati mifumo ya ulinzi ya Russia ilipokuwa inazuia mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani za Ukraine.

Lakini taarifa ya Kremlin haikusema kwamba Russia ndio iliitungua ndege hiyo, na kusisitiza tu kuwa kesi ya jinai imefunguliwa.

“Ndege hiyo ilitunguliwa kwa bahati mbaya,” Aliyev aliiambia televisheni ya serikali Jumapili.

“Kwa bahati mbaya, katika siku tatu za mwanzo tulisikia maelezo ya kipuuzi kutoka Russia,” Aliyev alisema.

Kiongozi huyo wa Azerbaijan alisema “Tumeshuhudia juhudi za wazi za kuficha ukweli kuhusu tukio hilo.”

Aliyev alisema anaitaka Russia kukiri ina hatia kwa kuitungua ndege hiyo na kwahusika waadhibiwe kwa uharibifu wa ndege uliosababisha vifo.

Forum

XS
SM
MD
LG