Ripoti hiyo imekusanya mahojiano na timu za madaktari na ustawi ambao waliwatibu zaidi ya mateka 100 wa Israel na wa kigeni, ambao wengi wao waliachiliwa mwishoni mwa mwezi Novemba 2023, kufuatia makubaliano ya muda mfupi ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas. Mateka wanane waliokolewa na jeshi la Israel.
Mateka hao ni pamoja na zaidi ya watoto 30 na vijana, wachache kati yao waligundulika wamefungwa kamba, kupigwa au kuchomwa na kitu cha moto, kulingana na ripoti iliyotumwa kwa Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mateso na kushapishwa Jumamosi jioni.
Forum