Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 04, 2025 Local time: 05:32

Jeshi la Ukraine limetungua ndege 21 zisizokuwa na rubani za Russia


Picha kutoka Maktaba ikionyesha mfano wa ndege zisizotumia rubani za Russia.
Picha kutoka Maktaba ikionyesha mfano wa ndege zisizotumia rubani za Russia.

Gavana wa Odesa, Oleh Kiper alisema kupitia mtandao wa Telegram vifusi vya Drone viliharibu majengo matano ya makazi.

Jeshi la Ukraine limesema leo Jumatatu kuwa limetungua ndege 21 zisizokuwa na rubani ambazo wanajeshi wa Russia walitumia katika mashambulizi ya usiku kucha yakilenga maeneo kadhaa kaskazini na mashariki mwa Ukraine.

Jeshi la anga la Ukraine limesema Russia ilirusha jumla ya ndege zisizokuwa na rubani 43, na kwamba ulinzi wake wa angani ulitungua ndege zisizo na rubani katika miji ya Chernihiv, Dnipropetrovsk, Donetsk, Kharkiv, Odesa na Poltava.

Gavana wa Odesa, Oleh Kiper alisema kupitia mtandao wa Telegram kwamba vifusi vya ndege zisizo na rubani viliharibu majengo matano ya makazi, lakini hayakumuumiza mtu yeyote. Gavana wa Kharkiv, Oleh Syniehubov aliripoti moto katika jengo uliosababishwa na shambulio la ndege isiyo na rubani ambayo iligonga karibu na barabara kuu.

Aliongeza kuwa hakuna majeruhi katika mkoa wake. Wizara ya ulinzi ya Russia imesema Jumatatu kuwa ilizuia ndege isiyokuwa na rubani katika eneo la Belgorod lililoko kwenye mpaka wa Russia na Ukraine.

Forum

XS
SM
MD
LG