Mangione aliondolewa kesi ya awali ya mashtaka ya Pennsylvania kwa mabadilishano na mwendesha mashtaka.
Wapalestina wakagua uharibifu wa majengo Gaza City.
Wawili hao Rosmah na Najib Razak wamekuwa wakikanusha kufanya makosa. Rosmah kwa sasa yuko huru kwa dhamana
Sudan inaitaka Uganda kuomba rasmi msamaha kutokana na kile imekitaja kuwa ujumbe wa kuchukiza na hatari ulioandikwa na mkuu wa jeshi la Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba, aliyetishia kuivamia Khartoum kijeshi.
Dominique Pelicot alikiri kosa la kumlewesha Gisele Pelicot na kumbaka na kuutoa mwili wake bila ridhaa kwa ajili ya ngono
Mahakama ya Juu ya Marekani, Jumatano imeamua kusikiliza maombi ya TikTok na kampuni yake mama ya China, ByteDance, kuzuia sheria iliyokusudia kulazimisha uuzwaji wa TikTo ifikapo Januari 19 au kupigwa marufuku kwa misingi ya usalama wa taifa.
Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, Jumatano amewataka wabunge wa Marekani kuukataa mswada wa ufadhili wa muda kwa bajeti baada ya Ijumaa, na hivyo kuongeza uwezekano wa kufungwa kwa sehemu ya serekali kuu.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, Jumatano amefanya mkutano na Seneta Mrepublikan, Marco Rubio, ambaye ametajwa na Rais mteule Donald Trump kuwa waziri ajaye wa mambo ya nje.
Tume ya uchaguzi nchini Chad imeliomba jeshi la taifa kusaidia kuwalinda maafisa wa uchaguzi na wagombea kuelekea uchaguzi wabunge na serikali za mitaa hapo Desemba 29.
Sehemu za kisiwa cha Mayotte kilicho chini ya usimamizi wa Ufaransa, zinaendelea kukadiria hasara kubwa leo Jumatano, baada ya kimbunga Chido kupiga kisiwa hicho jumamosi.
Kiongozi wa muungano wa kitaifa wa Syria Hadi al-Bahra, waliomuondoa rais Bashar Al-Assad amesema kwamba serikali ya mpito ya Syria inastahili kuhusisha kila chama cha Syria na wala sio kuwa na ubaguzi.
Mahakama ya juu nchini Ghana imetupilia mbali kesi mbili tofauti zilizokuwa zimewasilishwa kama rufaa kupinga mojawapo ya sheria kandamizi zaidi dhidi ya watu walio katika uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja.
Pandisha zaidi