Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 19, 2024 Local time: 22:09

Mahakama ya Malaysia imemuachia huru Rosmah Mansor


Rosmah Mansor (L) akiwa na mumewe Najib Razak, Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia katika picha iliyochukuliwa maktaba. Philippines, Nov. 12, 2017.
Rosmah Mansor (L) akiwa na mumewe Najib Razak, Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia katika picha iliyochukuliwa maktaba. Philippines, Nov. 12, 2017.

Wawili hao Rosmah na Najib Razak wamekuwa wakikanusha kufanya makosa. Rosmah kwa sasa yuko huru kwa dhamana

Mahakama Kuu ya Malaysia imemuachilia huru Rosmah Mansor, mke wa waziri mkuu wa zamani Najib Razak, kwa kosa la utakatishaji fedha na kukwepa kodi, ikieleza hakuna ushahidi wa kutosha wa kumfungulia mashtaka.

Najib na Rosmah wamekuwa chini ya uchunguzi mbali mbali wa rushwa tangu kushindwa kwa Najib katika uchaguzi wa mwaka 2018, wakati wapiga kura waliposhikwa na hasira juu ya jukumu lake katika kashfa ya mabilioni ya dola katika mfuko wa serikali wa 1Malaysia Development Berhad (1MDB) uliomaliza miaka yake tisa madarakani.

Wote wawili mara kwa mara wamekuwa wakikanusha kufanya makosa. Rosmah bado hajaepuka Sakata hilo, lakini kwa sasa yuko huru kwa dhamana akisubiri rufaa dhidi ya kifungo cha miaka 10 jela iliyotolewa mwaka 2022 kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ili kusaidia kampuni kushinda zabuni ya mradi wa usambazaji umeme wa jua, wa dola milioni 279 kutoka kwa serikali ya Najib.

Forum

XS
SM
MD
LG