Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari mjini Istanbul, Uturuki, Bahra amesema kwamba waakilishi wa muungano wa kitaifa wa Syria hawajakutana na kiongozi wa waasi wa Syria Ahmed al-Sharaa, lakini wamewasiliana na serikali ya mpito na washirika walio karibu naye.
Waasi wa Syria walidhibithi mji mkuu wa Damascus Desemba 8 na kumlazimu Assad kutoroka nchini baada ya miaka 13 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, na kumaliza utawala wa kifamilia wa miongo kadhaa.
Mapinduzi ya Syria yamesababisha hali ya wasiwasi, iwapo kutakuwa na ubadilishanaji wa Madaraka kwa njia ya utulivu.
Forum