Wahamiaji 27 wakiwemo wanawake na watoto, walifariki wakati boti mbili zilipopinduka kwenye pwani katikati mwa Tunisia, huku watu 83 waliokolewa, afisa wa ulinzi wa kiraia aliliambia shirika la habari la AFP siku ya Alhamisi.
Waandamanaji kadhaa walikusanyika katika mji wa Douma nchini Syria, Jumatano kudai majibu katika kutoweka kwa wanaharakati wanne mashuhuri waliotekwa nyara zaidi ya muongo mmoja uliopita.
Dereva mmoja aliendesha gari kwenye umati wa watu waliokuwa wakisherehekea Mwaka Mpya, Jumatano mapema mjini New Orleans na kufyatua risasi, na kuuwa watu 10 pamoja na kujeruhi wengine zaidi ya 35 katika shambulizi FBI imesema inachunguza kama kitendo cha kigaidi.
Rais Joe Biden wa Marekani ametoa maelezo mafupi kuhusiana na tukio na mauajai na majeruhi la New Orleans kabla ya kuondoka Wilmington, Delaware.
Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara alisema katika hotuba yake ya mwisho wa mwaka kwamba wanajeshi wa Ufaransa wataondoka katika taifa hilo la Afrika Magharibi mwezi huu wa Januari.
Maafisa wa Palestina wamesema mashambulizi ya anga ya Israel kaskazini na kati kati mwa Gaza yamesababisha vifo vya watu 15.
Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara katika hotuba yake ya mwisho wa mwaka anataka wanajeshi wa Ufaransa kuondoka katika taifa hilo la Afrika Magharibi kuanzia mwezi wa kwanza.
Watu kumi waliuawa na 35 kujeruhiwa baada ya mshukiwa kuvurumisha gari lake kwenye umati wa watembea kwa miguu katika Barabara yenye shughuli nyingi ya French Quarter huko New Orleans leo saa tisa na robo alfajiri siku ya Jumatano kwenye mtaa wa Bourbon.
Rais wa Kenya, William Ruto, Jumanne amekiri ukiukaji unaofanywa na vikosi vya usalama vya Kenya, kufuatia maandamano dhidi ya wimbi la karibuni la tuhuma za utekaji ambalo limezua ghadhabu nchini humo.
Sudan Kusini inapanga kuanza tena uchimbaji mafuta ghafi baada ya mapigano yanayoendelea katika nchi jirani ya Sudan kusababisha uharibifu kwenye bomba la kusafirisha mafuta mapema mwaka huu.
Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema leo Jumanne kwamba imetoa taarifa muhimu na utafiti wa hivi karibuni kuhusu virusi vya Corona kwa jamuiya ya kimataifa na kwamba kazi ya kutafuta chanzo cha mlipuko wa virusi hivyo unastahili kufanyika katika nchi nyingine.
Waziri mkuu wa Ufaransa Francois Bayrou ameahidi msaada zaidi kwa watu wa kisiwa cha Mayitte, akiwa katika ziara hii leo kwenye kisiwa hicho katika Bahari hindi ambapo ameahidi ujenzi mpya, kufuatia uharibifu uliosababishwa na kimbunga Chido.
Pandisha zaidi