Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 06, 2025 Local time: 18:30

China inataka uchunguzi kuhusu Corona kufanyika kwingine


Picha inayoonyesha namna virusi vya Corona vilivyo
Picha inayoonyesha namna virusi vya Corona vilivyo

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema leo Jumanne kwamba imetoa taarifa muhimu na utafiti wa hivi karibuni kuhusu virusi vya Corona kwa jamuiya ya kimataifa na kwamba kazi ya kutafuta chanzo cha mlipuko wa virusi hivyo unastahili kufanyika katika nchi nyingine.

Taarifa hiyo imetolewa baada ya Shirika la Afya Duniani kutaka China kutoa maelezo na kuruhusu uchunguzi kufanyika kuhusu kilichosababisha mlipuko wa virusi vya Corona.

Maambukizi ya kwanza ya virusi vya Corona yaliripotiwa China, miaka mitano iliyopita.

Msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesema katika kikao na waandishi wa habari kwamba China iko tayari kushirikiana na kila mshirika katika utafiti wa kisayansi kote duniani na kutoa mchango muhimu katika kuzuia mlipuko wa magonjwa hatari katika siku zijazo.

Forum

XS
SM
MD
LG