Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 04, 2025 Local time: 18:56

10 wauwawa New Orleans katika shambulizi FBI inachunguza kuwa la kigaidi


Dereva mmoja aliendesha gari kwenye umati wa watu waliokuwa wakisherehekea Mwaka Mpya, Jumatano mapema mjini New Orleans na kufyatua risasi, na kuuwa watu 10 pamoja na kujeruhi wengine zaidi ya 35 katika shambulizi FBI imesema inachunguza kama kitendo cha kigaidi.

Mshukiwa aliuwawa baada ya majibizano ya risasi na polisi, maafisa usalama wamesema.

“Mtu huyo alikuwa akijaribu kuwagonga watu wengi kadri iwezekanavyo,” mkuu wa polisi wa New Orleans, Anne Kirkpatrick amesema Jumatano katika mkutano na waandishi wa habari.

New Orleans ni kivutio cha kihistoria cha watalii na huwa na baa na muziki, katika eneo hilo, ambapo pia linajulikana kwa mkesha wake mkubwa wa Mwaka Mpya.

Forum

XS
SM
MD
LG