Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 04, 2025 Local time: 14:53

Rais Biden atoa maelezo kuhusu mauaji ya New Orleans


Rais Joe Biden wa Marekani
Rais Joe Biden wa Marekani

Rais Joe Biden wa Marekani ametoa maelezo mafupi kuhusiana na tukio na mauajai na majeruhi la New Orleans kabla ya kuondoka Wilmington, Delaware.  

Kulingana na ikulu ya White house, Rais Biden alimpigia simu Meya wa New Orleans La Toya Cantrell asubuhi ya Jumatatu kutoa msaada wa serikali kufuatia habari mbaya kwamba dereva aliuwa na kujeruhi watu katika Mji wa New Orleans.

Hata hivyo Rais Biden amepewa taarifa za hivi karibuni na uongozi mkuu wa FBI na DHS na timu yake ya usalama wa nchi na ataendelea kufahamishwa kuhusu tukio hilo siku nzima.

Watu 10 wameuwawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa wakati gari lilipoendeshwa katika kundi kubwa la watu kwenye mji wa New Orleans katika eneo maarufu ya French Quarter katika saa za kwanza za siku ya mwaka mpya .

Shirika la NOLA Ready idara inayosimamia maswala ya dharura lilitoa tahadhari kwamba polisi walikuwa wanajibu tukio lililodhuru watu wengi katika mitaa ya Canal na Bourbon.

Polisi wamesema gari kubwa liliendeshwa kwa kasi na kisha dereva akatoka nje na kuanza kuwafyatulia watu risasi , huku polisi wakijibu kwa risasi.

Mkuu wa polisi wa New Orleans Anne Kirkpatrick aliwaambia waandishi wa habari kwamba maofisa wawili wa polisi walipigwa risasi na kujeruhiwa katika mapambano hayo.

Amesema tukio hilo lilikuwa ni la makusudi.

Tukio hilo limekuja saa chache kabla ya kuanza mchezo wa Sugar Bowl ambao moja michezo kadhaa ya michuano ya kitaifa ya college football, ambapo inakadiriwa kulikuwa na watu zaidi elfu 60 waliohudhuria.

Forum

XS
SM
MD
LG