Maelfu ya wafungwa wametoroka jela kubwa jamhuri ya kidemokrasi ya Congo mashariki mwa mji wa Goma mapema Jumatatu, Katikati ya mapigano ya waasi kwenye mji , mlinzi wa wafungwa na mkaazi wamesema.
Mshtuko wa masoko ya fedha umetokea China ambapo kampuni moja imetengeneza app inayoshindana na kampuni kubwa za Marekani
Mwanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo amesema hali ni ngumu sana na wanajeshi wanapambana bila mafanikio huku vikosi vya waasi vikisonga mbele, hiyo ni kwa mujibu wa video iliyotumwa katika mtandao wa kijamii Jumatatu.
Maelfu ya watu wengi wao wakitembea kwa miguu walikuwa barabarani kuelekea Gaza City ambayo imeshuhudia uharibifu katika vita.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumapili limewataka waasi wa M23 kusitisha mashambulizi yao na kuacha kusonga mbele kuelekea mji wa Goma, mji mkubwa wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kuomba majeshi ya kigeni kuondoka mara moja.
Rais wa Marekani Donald Trump Jumapili alisema kwamba ameamuru ushuru, marufuku ya viza na hatua nyingine za ulipizaji kisasi zichukuliwe dhidi ya Colombia baada ya serikali ya nchi hiyo kuzikatilia ndege mbili zilizokuwa zinabeba wahamiaji kuingia nchini humo.
Wapiganaji wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Kiislamu waliwaua wanajeshi 20 wa Nigeria, akiwemo kamanda mmoja, baada ya kushambulia kambi ya kijeshi katika mji wa mbali kaskazini mashariki mwa jimbo la Borno, vyanzo vya usalama na wakazi walisema Jumapili.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Jumapili ametoa mwito kwa vikosi vya Rwanda kuondoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kusitisha msaada kwa wapiganaji wa M23 wanaosonga mbele katika mji wa Goma.
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imekata uhusiano wa kidiplomasia na Rwanda huku mapigano kati ya waasi wanaoungwa mkono na Rwanda na vikosi vya serikali yakiendelea kuzunguka mji muhimu wa mashariki wa Goma.
Hali ya wasi wasi inazidi kuongezeka katika Mji wa Goma kufuatia mapigano makali yanayoendelea pembezoni mwa mji wa Goma.
Ripoti za raia wa China waliosafirishwa katika vituo vya ulaghai kwenye mpaka wa Thailand na Myanmar zinaibua maswali mapya kuhusu utegemezi wa Beijing kwa utawala wa kijeshi wa Myanmar kukabiliana na uhalifu wa kimataifa.
Hamas ilipanga Jumamosi kuwaachilia wanawake wanne raia wa Israeli waliokuwa wakishikiliwa mateka kubadilishana na wafungwa wa Kipalestina katika makubaliano ya pili ya kusitisha mapigano huko Gaza.
Pandisha zaidi