Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 08:08

Wafungwa watoroka gerezani DRC


Wanajeshi wa FARDC wakifanya operesheni huko Kivu Kaskazini Decemba 17, 2024. Picha na AFP
Wanajeshi wa FARDC wakifanya operesheni huko Kivu Kaskazini Decemba 17, 2024. Picha na AFP

Video ya mtu aliyeshuhudia iliyobandikwa katika mtandao wa kijamii imeonyesha kundi la wafungwa likikimbia kutoka Jela na moshi ukifuka kutoka ndani ya majengo.

Reuters iliweza kuthibitisha mahali pa majengo hayo , uzio , miti na eneo lenyewe katika video ambayo ilioanishwa na picha za satelite. Wanaume wanaonekana katika video wanaondoka katika jela lakini utambulisho wao haukuweza kuthibitishwa haraka.

Waasi wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda waliingia katika mji mkubwa wa Goma mashariki mwa Congo na vikosi vya afrika mashariki vilishambulia kwa risasi kwenye mpaka katika mzozo unaoelezewa kuwa mkubwa kwa zaidi ya muongo mmoja.

Wakati huo huo, katika kituo cha mpakani cha Gisenyi, Rwanda, mamia ya watu, wakiwemo wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, wanakimbia mapigano makali katika mji uliozingirwa wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya kusonga mbele kwa wapiganaji wa kundi la waasi la M23, na wanajeshi wa Rwanda kuingia katika mji huo mkuu wa eneo hilo.

Kikosi cha kulinda amani cha MONUSCO kikiwaondoa wafanyakazio wa UN huko Goma DRC Januari 25, 2025. Picha na Reuters
Kikosi cha kulinda amani cha MONUSCO kikiwaondoa wafanyakazio wa UN huko Goma DRC Januari 25, 2025. Picha na Reuters

Wanajeshi wa Kongo waliojisalimisha wanaonekana wakiandamana na wanajeshi wa Rwanda kwenye kituo hicho cha mpakani.

Mji wa Goma ulitikiswa na sauti za silaha nzito siku ya Jumatatu huku Ufaransa ikisema kwamba mji huo ulikuwa katika hatari ya kuwa chini ya udhibiti wa wanamgambo na wanajeshi wa Rwanda.

Kundi la waasi la M23 na wanajeshi wa Rwanda waliingia katikati mwa Goma Jumapili usiku baada ya wiki kadhaa za kusonga mbele kuelekea mji huo mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, wenye utajiri wa madini nchini DR Congo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot alisema mashambulizi yanayoungwa mkono na Rwanda "lazima yakome", akielezea mshikamano wa nchi yake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Huku shinikizo la kimataifa likiongezeka la kutaka kumalizika kwa vita vya Goma, Kenya ilitangaza Jumapili kwamba Rais wa Kongo Felix Tshisekedi na Rais wa Rwanda Paul Kagame wamekubali kuhudhuria mkutano wa kilele katika siku mbili zijazo.

Wapiganaji wa M23 na wanajeshi 3,000 hadi 4,000 wa Rwanda walikuwa wameizingira Goma kwa siku kadhaa, kulingana na Umoja wa Mataifa na vyanzo vya usalama.

Wanajeshi wa Kongo wanaonekana kuzidiwa nguvu na mashambulizi hayo, na jeshi la Uruguay lilisema katika taarifa yake kwamba baadhi ya vitengo vimeanza kujisalimisha kwa kukabidhi silaha zao kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Goma.

Mpaka kati ya Rwanda na DRC karibu na Goma pia ulifungwa siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa chanzo cha ubalozi wa Ulaya na mfanyakazi mmoja wa misaada katika mpaka huo.

Forum

XS
SM
MD
LG