Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 30, 2025 Local time: 11:25

DRC yakata uhusiano na Rwanda


Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) President Felix Tshisekedi.
Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) President Felix Tshisekedi.

Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imekata uhusiano wa kidiplomasia na Rwanda huku mapigano kati ya waasi wanaoungwa mkono na Rwanda na vikosi vya serikali yakiendelea kuzunguka mji muhimu wa mashariki wa Goma.

Mapigano yamesababisha walinda amani 13 na wanajeshi wa kigeni kuuawa na maelfu ya raia kuyahama makaazi yao.

Kundi la waasi la M23 limepata mafanikio makubwa katika eneo la mpaka na Rwanda katika wiki za hivi karibuni, na kuifunga Goma, mji mkuu wa jimbo wa takriban watu milioni 2 na kitovu cha kikanda cha usalama na juhudi za kibinadamu.

DRC, Marekani na wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaishutumu Rwanda kwa kuunga mkono M23, ambayo inaundwa zaidi na Watutsi ambao walijitenga na jeshi la Congo zaidi ya miaka kumi iliyopita.

Ni mojawapo ya makundi yapatayo 100 yenye silaha ambayo yamekuwa yakigombea nafasi katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini, ambapo mzozo wa muda mrefu umezua moja ya migogoro mikubwa zaidi ya kibinadamu duniani.

Forum

XS
SM
MD
LG