Guterres, ameredia kulaani vikali uvamizi unaoendelea wa kundi la M23 na kusonga mbele kuelekea Goma, Kivu Kaskazini kwa msaada wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda, msemaji Stephane Dujarric, amesema katika taarifa yake.
“Anatoa wito kwa M23 kusitisha mara moja vitendo vyote vya uhasama na kuondoka katika maeneo yanayokaliwa.
Anatoa wito zaidi kwa Vikosi vya Ulinzi vya Rwanda kusitisha msaada kwa M23 na kuondoka katika eneo la DRC,” Dujarric amesema.
Hapo awali mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa aliongelea tena ripoti ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa iliyotaja uungaji mkono wa Kigali kwa wapiganaji wa M23, kundi linaloipinga serikali na kupigana na jeshi la DRC mashariki mwa nchi hiyo.
Forum