Wanawake hao wanne ni Karina Ariev, Daniella Gilboa, Naama Levy na Liri Albag, Hamas ilisema Ijumaa. Wanawake wote hao wanne ni wanajeshi wa Israel waliotekwa nyara kutoka katika kambi ya Nahal Oz kusini mwa Israel Oktoba 7, 2023, wakati Hamas ilipofanya shambulizi lake.
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ilithibitisha kuwa imepokea orodha hiyo kupitia wapatanishi na kwamba majibu yake yatatolewa baadaye.
Forum