Hali ya wasi wasi inazidi kuongezeka katika Mji wa Goma kufuatia mapigano makali yanayoendelea pembezoni mwa mji wa Goma.
Ripoti za raia wa China waliosafirishwa katika vituo vya ulaghai kwenye mpaka wa Thailand na Myanmar zinaibua maswali mapya kuhusu utegemezi wa Beijing kwa utawala wa kijeshi wa Myanmar kukabiliana na uhalifu wa kimataifa.
Hamas ilipanga Jumamosi kuwaachilia wanawake wanne raia wa Israeli waliokuwa wakishikiliwa mateka kubadilishana na wafungwa wa Kipalestina katika makubaliano ya pili ya kusitisha mapigano huko Gaza.
Wanajeshi wa DRC walizuia jaribio la waasi wanaoungwa mkono na Rwanda usiku kucha katika mji wa Goma, mashariki mwa nchi hiyo vyanzo viwili vya jeshi la Congo vilisema Jumamosi, baada ya sauti za mashambulizi makubwa ya mabomu kuutikisa mji huo saa za alfajiri.
Waasi wa Kihouthi wa Yemen wamewakamata wafanyakazi wengine saba wa Umoja wa Mataifa, mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema Ijumaa, hiyo ni hatua yao ya hivi karibuni ya kuwalenga wafanyakazi wa misaada.
Rais wa Moldova Maia Sandu aliitembelea Kyiv Jumamosi kwa mazungumzo na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy huku mivutano inaoongezeka huko Transnistria, eneo linaloliunga mkono Russia kutaka kujitenga la Moldova ambalo ni jirani na Ukraine.
Shambulizi la ndege isiyo na rubani kwenye moja ya hospitali za mwisho zinazofanya kazi huko El-Fasher katika jimbo la Darfur nchini Sudan liliuwa watu 30 na kujeruhi kadhaa, chanzo cha watabibu kilisema Jumamosi.
Hali ya wasiwasi iliendelea kutanda Jumamosi katika maeneo kadhaa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufuatia kifo cha gavana wa kijeshi wa Kivu Kaskazini siku ya Ijumaa.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema Alhamisi kwamba hivi karibuni atazungumza na mwezake wa Russia Vladimir Putin ili kujaribu kumshinikiza amalize vita vilivyodumu kwa karibu miaka mitatu na jirani yake Ukraine.
Wabunge wa Marekani Alhamisi wamewasilisha msuada unaolenga kusitisha hadhi maalum ya kibiashara kwa China na Marekani, kuongeza ushuru kwa kiwango cha juu, pamoja na kumaliza sera ya kutolipiwa ushuru kwa bidhaa za thamani ndogo kutoka China.
Rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh amesema ana nia ya kuchukua tena udhibiti wa chama chake cha siasa na kutangaza kwamba “anarudi nyumbani”, katika ujumbe wa sauti ambao shirika la habari la AFP limeupata Alhamisi.
Moto mwingine wa nyika umejitokeza na kusambaa kwa kasi katika eneo moja kaskazini mwa Los Angeles Jumatano ukiongezeka kutokana na upepo mkali na hali ya ukavu.
Pandisha zaidi