Waasi wa Kihouthi wa Yemen wamewakamata wafanyakazi wengine saba wa Umoja wa Mataifa, mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema Ijumaa, hiyo ni hatua yao ya hivi karibuni ya kuwalenga wafanyakazi wa misaada.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kuachiliwa huru mara moja na bila masharti wafanyakazi wote wa misaada wanaoshikiliwa nchini Yemen, ambayo inakabiliwa na moja ya majanga makubwa zaidi ya kibinadamu duniani.
Waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran wamewakamata darzeni ya wafanyakazi kutoka Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kibinadamu, wengi wao tangu katikati ya mwaka jana.
Forum