Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 03:52

Moto mwingine umejitokeza na kuongezeka  kaskazini mwa Los Angeles

Magari ya dharura yapo kando ya barabara huku miali ya moto kutoka mbio za Hughes Fire ikipanda mlima Castaic, kitongoji cha kaskazini-magharibi mwa Los Angeles, California, Januari 22, 2025.
Magari ya dharura yapo kando ya barabara huku miali ya moto kutoka mbio za Hughes Fire ikipanda mlima Castaic, kitongoji cha kaskazini-magharibi mwa Los Angeles, California, Januari 22, 2025.

Moto mwengine wa nyika umejitokeza na kuongezeka  kwa kasi katika eneo moja kaskazini mwa Los Angeles Jumatano ukiongezeka kutokana na upepo mkali na hali ya ukavu.

Moto mwengine wa nyika umejitokeza na kuongezeka kwa kasi katika eneo moja kaskazini mwa Los Angeles Jumatano ukiongezeka kutokana na upepo mkali na hali ya ukavu.

Katika saa chache , moto uliongezeka kufika hadi theluthi mbili kwa ukubwa wa ule Moto wa Eaton moja ya moto mkubwa ulioharibu maeneo kadhaa ya mji.

Mkuu wa polisi wa kaunti ya Los Angeles alisema kwamba watu 31,000 walitakiwa kuhama na wengine elfu 23 walipewa onyo la kuondoka kutoka makazi yao.

Moto mpya umesababisha ugumu kwa wafanyakazi wa zimamoto ambao wamekaribia kudhibiti moto mkubwa katika maeneo mengine mawili ya eneo hilo .

Idara ya misitu ya California na udhibiti wa moto imesema takriban wafanyakazi 1,100 wa zimamoto wamepelekwa kusini mwa California kupambana na moto uliokuwa unaendelea kwa kasi.

Forum

XS
SM
MD
LG