Msuada huo uliowasilishwa na John Moolenaar ambaye ni mwenyekiti wa kamati maalum ya wawakilishi wa Repablikan, kwa ajili wa China kwenye baraza la wawakilishi, umekuja baada ya rais Donald Trump kutoa waraka Jumatatu akiomba bunge kutathmini sheria ya Uhusiano wa Biashara wa Kudumu, PNTR na Beijing.
Sheria hiyo ilipitishwa na bunge la Marekani mwaka 2000 na kufungua njia kwa China kujiunga na Shirika la Kimataifa la Biashara. Hata hivyo Marekani mara kadhaa imegundua uingiliaji mkubwa wa serikali kwenye uchumi wa China ikiwemo ruzuku kubwa kwa baadhi ya makampuni kinyume na sheria za WTO.
Trump ambaye amekuwa akilalamikia ukosefu wa usawa kwenye biashara kati ya Marekani na China ameapa kuongeza ushuru kwenye bidhaa za China. Haijabainika njia itakayotumika kuelelekea kuidhishwa kwa msuada huo kuwa sheria, ingawa Warepablikan wana wingi kwenye bunge la Senate na la Wawakilishi na kwa hivyo kuufanya rahisi kupita.
Ubalozi wa China hapa Washington haujasema lolote kuhusu hilo hata baada ya kuombwa kufanya hivyo.
Forum