Kwenye siku yake ya kwanza ofisini, alibatilisha amri ya kiutendaji iliyotiwa saini 2023 na rais Joe Biden ikilenga kudhibiti mwendelezo wa AI yenye nguvu zaidi, na badala yake kuweka mikakati ya kuhakikisha ubinafsi unalindwa, haki za kijamii pamoja na usalama wa kitaifa.
Siku iliyofuata Trump alikutana na viongozi wa makampuni makubwa ya teknolojia akiwemo Sam Altman, Mkurugenzi mkuu wa Open AI, Larry Ellison, mwenyekiti wa Oracle na Masayoshi Son, Mkurugenzi mkuu wa SoftBank, na kutangaza uwekezaji wa dola bilioni 500 kwenye mfumo wa AI unaojulikana pia kama Stargate.
Stargate inalenga kuwekeza katika kubuni hadi vituo 10 vikubwa vya data hapa Marekani ambavyo vitatoa huduma za kompyuta kwa mifumo ya AI. Kituo cha kwanza tayari kinajengwa Texas. Uwekezaji huo unatarajiwa kuunda hadi ajira 100,000 wakuu wa makampuni hayo wamesema.
Forum