Dhoruba ya theluji, barafu, upepo na kushuka kwa viwango vya hali ya hewa nchini Marekani kumesababisha hali ya hatari.
Makamu wa rais wa zamani wa Ecuador Jorge Glas, ameondolewa kutoka gerezani baada ya jaribio kwa maisha yake, wakili wake Sonia Gabriela Vera, amesema Jumapili, wakati akiilaumu serikali kwa hali hiyo.
Hali hatari sana ya hewa ya baridi Jumapili imekumba eneo kubwa la kati kati mwa Marekani, huku dhoruba kali ikielekea upande wa mashariki, na kusababisha usumbufu kwa usafiri na kazi kutoka Kansas City hadi Washington DC.
Hati ya kumkamata Yoon kwa misingi ya kufanya uasi inatarajiwa muda wake kumalizika usiku wa manane siku ya Jumatatu.
Wadhifa wa Sarkozy umegubikwa na matatizo ya kisheria tangu aliposhindwa uchaguzi wa rais mwaka 2012.
Wapigana wa Wagner wamekuwepo nchini Mali tangu jeshi lilipokamata madaraka katika mapinduzi ya mwaka 2020 na 2021
Meloni alionekana mshirika mwenye nguvu kwa Trump kutokana na yeye kuwa M-conservative na mrengo wa kulia huko Italy.
Mwanadiplomasia wa Syria na afisa wa Qatar wameithibitisha AFP imefanya mkutano na waziri wa muda wa mambo ya nje wa Syria
Serikali ya kijeshi ya Myanmar imewaachia huru zaidi ya wafungwa 6,000 na kupunguza adhabu za vifungo vya wafungwa wengine, kama sehemu ya msamaha kwa watu wengi katika kuadhimisha miaka 77 ya uhuru wake kutoka kwa Uingereza siku ya Jumamosi.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz katika mahojiano yaliyochapishwa Jumamosi , amelaani matamshi “ ya ovyo ” ya Elon Musk na msimamo wake wa wazi kukiunga mkono chama cha mrengo mkali wa kulia cha AfD.
Wizara ya ulinzi ya Russia Jumamosi imesema wanajeshi wa Russia wamedhibiti kijiji cha Nadiya katika mkoa wa mashariki mwa Ukraine wa Luhansk na kutungua makombora manane yaliyotengezwa Marekani aina ya ATACMS.
Pandisha zaidi