Mawaziri wa serikali ya mpito ya Syria wameisihi Marekani kuondoa vikwazo kwa Damascus wakati wa ziara yao ya kwanza nchini Qatar tangu kuangushwa kwa Rais Bashar al-Assad.
Katika taarifa wizara ya mambo ya nje ya Syria imesema nchi hiyo ya Ghuba imefanya mkutano wake wa kwanza na waziri wa muda wa mambo ya nje wa Syria, Asaada al-Shaibani, waziri wa ulinzi Murhaf Abu Qasr ana mkuu mpya wa upelelezi, Anas Khattab. Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al-Thani, ‘ameelezea msimamo wa serikali ya Qatar kuiunga mkono Syria kwa umoja, uhuru na mshikamano,’ taarifa imesema.
Awali mwanadiplomasia wa Syria na afisa wa Qatar wameithibitisha AFP kuwa Shaibani aliwasili Jumapili asubuhi kwa mikutano huko Qatar, mwenyeji wa kambi kubwa ya kijeshi ya Marekani katika kanda hiyo. Kinyume na nchi nyingine za Kiarabu, Qatar haijawahi kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Syria chini ya Assad ambaye aliangushwa na uasi wa siku 11 ambao ulisonga mbele na kuingia katika miji mikubwa na halafu kuingia mji mkuu Damascus mwezi Desemba.
Kufuatia majadiliano na Waziri wa Nchi wa Qatar, Mohammed bin Abdulaziz Al-Khulaifi, Shaibani alirejea wito wake wa kuondoa vikwazo vya Marekani kwa Syria.
Forum