Tajiri huyo mkubwa sana duniani, mmliki wa mtandao wa kijamii wa X, katika msururu wa maoni yake katika siku za hivi karibuni aliwashambulia viongozi kadhaa wa Ulaya na kuzua gumzo katika bara hilo.
Alipoulizwa kuhusu uingiliaji kati wa Musk, ambaye mwezi uliopita alimuita Scholz “mpumbavu asiye na uzoefu” kabla ya kumuita rais wa Ujerumani “mkandamizaji wa demokrasia”, Kansela Scholz aliliambia jarida la Stern kuwa ni muhimu “kutulia” kabla ya uchaguzi wa mapema wa Ujerumani utakaofanyika tarehe 23 Februari.
“Nchini Ujerumani, kila kitu kinakwenda kulingana na matakwa ya raia na sio maoni ya ovyo ya bilionea wa Marekani,” aliliambia jarida hilo katika mahojiano.
Forum